Breaking

Saturday, April 18, 2020

Unamtongoza, Anasema Anakuchukulia Kama Rafiki, Unajua Kwanini?


“Hataki muwe zaidi ya hapo, anakuchukulia kama rafiki!”
Stori inakwenda hivi; baada ya kumwangalia kwa muda mrefu, huyumwanamke anambae anakuuwa pole pole kwa mvuto wake, ambae anakila kitu ambacho wewe macho yako kwako unaona ndo kile kinachoitwa na kutengeneza uzuri usiopimika, ubongo wako unaamini ya kuwa mnaendana kwa kila kitu ila kinachokuchanganya ni wewe kutokua na uhakika iwapo na wewe unampendeza yeye, Kijana wa watu unajituma na kupiga moyo konde, leo hii unajikaza kiume na kwenda kumwambia yale yote yaliyo moyoni mwako… mara… ‘kwaaa…’ anakujibu, “Oho, lakini mbona mie siku zote huwa nakuona na kukuchukulia kama rafiki, kama rafiki.. rafiki tu!”, moyo unapigwa na radi ya maumivu, na huamini kilichokupata, huku kichwani sauti ya “kama rafiki” ikijirudia rudia!.
Kama kungekua na kitu cha kuzuia hii dhihaka, ungetumia na kurudisha muda nyuma, kiume.com tumekusanya dalili zote za kuangalia kabla ya kupiga moyo kode na kwenda kumwambia yanayokusibu moyoni…
Anajiamini sana akiwa na wewe mpaka mazoea yake yamepitiliza…Msichana akiwa anajiamini sana kwako, ujue hapo umeshapoteza unachotamani na umeishia kunawa, kwa msichana akimuona mtu anayempenda kweli, utaona dalili…!, utaona hatulii, mara akae vizuri, na anakua anajihisi tu mda wote, atashika nywele zake kuangalia kama ziko vizuri, mapenzi asikuambie mtu kaka, mapenzi yanaleta kutokujiamini, na iwapo anajiamini sana kwako na ashtuki akikuona, wala atikisi hata ukucha basi hapo tafuta kitu kingine tu cha kufanya.
Anakupa hadithi za wanawake wengine… Msichana ambae yupo singo hana mpenzi, halafu ukiwa nae anakua anakupa stori za wasichana wengine, hapo anatumia janja ya nyani, hapo anakubadilisha akili usimwazie yeye na uwawazie hao wasichana wengine anaokupigisha stori, achana kabisa na haya maongezi, anaweza kukwambia.. “ooho, unaonaje nikikupigia pande kwa rafiki yangu Janeti, si ni mzuri eeh?”, kaka hapo unapoteza mda tu.
Hafanyi kile unachotaka…Ukiona msichana hasikilizi kile unachotaka, yeye siku nzima anakuomba umsaidie hichi, twende pale.., we ukimwambia ya kwako anaruka maili tisa, ujue hapa huna chako, we upo pale ili akutumie tu na kwa sababu hana hisia nawe hajiulizi hata huyu jamaa anajisikiaje!.
Anatukana bila kujari uwepo wako…Maneno anayotumia ni kama yupo namwanamke mwenzie, na wala hashituki!, kaka hapa umeshakwenda na maji, mapenzi yana heshima na anayekupenda huwa anashituka akiona tu uwepo wako, na aibu yake sikuzote hua ipo karibu.
Hataki kuonekana na wewe sehemu za wazi…Ukimwambia tutoke wote, anakua na visingizio. Ukimwambia twende wote nikusindikize uendako, hata kama ni sokoni… utamsikia “ohhoo, mi nilishazoea kutembea mwenyewe wakati wote, mama atanielewa vibaya”. Hapa ni kwamba anaogopa utamwalibia chansi ya kukutana na mwanaume wa ukweli achana na wewe masuruali tu, mama gani ambae hapendi mwanae aolewe?.
Anakuomba misaada mda wote…  Msichana mwenye hisia nawe hawezi kukuomba misaada ovyo hovyo, kwanza atakua hajiamini na hujiuliza maswali kama “Hivi atanionaje na atajifikiliaje nikimuomba hiki?”.
Anakufanya kama spea tairi…Siku akikubali kutoka mtoko nawe, utashangaa kaja na mashoga zake!, hii anakua anafahamu kabisa kwa hio anakua anajihami ili usije ukapata chansi ya kuwa wewe na yeye. Yeye saa zote ni vicheko tu…, kidogo tu mara anaenda chooni, mwisho wa siku mbaba unaagwa usiku umeingia sie tunaenda.
hafanyi michezo yeyote ya kuwa karibu nae…Mwanamke akikupenda anatamani saa zote awe karibu nawe, mara mjikute mmeshikana mikono mda mrefu mpaka jasho, sasa huyu yeye atakua anakulia taimingi, anakua anahakikisha hakuna mguso wa ajabu ajabu, kaka mguso huleta hisia, na kama hana hisia kwako hawezi kufanya hivyo.
Anaongea na wanaume wengine mbele yako…Hivi hili si linaonekana kabisa, hili halina haja hata la kuliongelea, ila mtu akiwa amependa inawezekana kabisa asilione hata hili, anakua anajipa matumaini hewa!, huku kichwani akilipa sababu nyingine kabisa, “Oooh yuko sosho sana!”.Kaka hapo kama msemo wa kiumeni.com usemavyo, “umeshaliwa kekundu”.
Hakutambulishi kwa rafiki zake…Hana hisia nawe atakutambulisha kwa nini?, labda kwa sababu vocha zote zinatoka kwako!, samahani kwa kuongea hivi najua nakukera ila ndo ukweli wenyewe, na hata ukitambulishwa, utatambulishwa kama rafiki tu, na hivyo ndo utabaki kuwa.
Cha kufanya jiongeze, na hata kama yeye ndo huwa anakupigia simu au anakufata na anaonyesha hisia ujue kuna kitu zaidi ya wewe kinachoendelea kumweka kwako.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment