Breaking

Thursday, April 2, 2020

Vanessa Mdee kavunja ukimya, Rotimi kasisitiza “Hatuachani”Mwimbaji Staa wa Bongofleva Vanessa Mdee amevunja ukimya kwa kuongelea ukimya wake na maamuzi yake ya kupumzika.

“Kwa miaka 13 nimefanya kazi bila mapumziko, hatimae nimepata muda kwa ajili yangu, kufanya ninavyovipenda na kuvitaka, nataka kuchukua muda kufurahia maisha, tuko hapa kwa ajili ya kuishi na kufurahia maisha” – Vanessa Mdee 

Wakati Vanessa akiongea kwenye hii video na kuonesha kufurahia penzi lake jipya na Mwigizaji Staa Rotimi, Mpenzi wake huyo alijitokeza na kuongea kwa kiswahili kurudia kwa msisitio neno ‘hatuachani’

Vanessa amewashukuru Mashabiki zake pia kwa kusupport podcast yake kwenye season ya kwanza na kuahidi kuileta season ya pili na kujibu maswali mengi ya Mashabiki zake.

Bonyeza PLAY hapa chini kutazama VIDEO.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE 

No comments:

Post a Comment