Breaking

Saturday, April 18, 2020

VIDEO: Hawa ni Kina Nani? Nimekuwekea Hapa Historia Yao Kwa Ufupi


HAWA NI KINA NANI?

Siku za hivi karibuni utakuwa umekutana na video za hawa jamaa ambao kila mtu amewapa jina lake wengine wanawaita kamati ya roho mbaya, wengine *Wajuba na majina mengine.

NI KINA NANI?: Wanatokea nchini Ghana, ambako ni utamaduni wao kufanya mazishi yakiambatana na sherehe. Kundi unaloona linatrend sana siku hizi liliundwa mwaka 2010. Kiongozi wao ni Benjamin Aidoo, ambaye kwa sasa ni 'star' huko Ghana.

Mwaka 2017 Benjamin alifanya mahojiano na *BBC, akaeleza kwamba "Watu wa Ghana wathamini zaidi waliokufa kuliko walio hai,...". Yeye aliongeza thamani kwenye biashara yake ya majeneza, akabuni mitindo ya kucheza. Mteja akienda anaambiwa achague anataka mtu wake azikweje, na wengi huchagua wapendwa wao wasindikizwe kwa mbwembe za kucheza. Ule wimbo (Astorominia) unaotumika kwenye video zao za mtandaoni umeongezwa tu, nyimbo tofauti tofauti hutumika misibani.

WANAPIGA HELA : Huko Ghana watu wanakopa benki ili wafanye sherehe za mazishi, mtu kununua jeneza kwa milioni ni jambo la kawaida tu. Aidoo hutoa huduma yake kwa mtonyo kuanzia cedis 2,220 (Kama shilingi 883,754.)

Iko hivyo: sasa tuwape jina gani, WAJUBA linafaa?

VIDEO:

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment