Breaking

Friday, April 3, 2020

Virusi vya Corona: Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona Kenya yapanda hadi 110

Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona (Covid-19) nchini Kenya imefikia 110 baada ya watu wengine 29 kuthibitishwa kuwa navyo ndani ya saa 24 zilizopita.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari jijini Nairobi waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kwamba watu wengine wawili wamepoteza maisha yao kutokana na maambukizi ya virusi hivyo.

Amesema kwamba idadi hiyo inaongeza idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo kufikia watatu. Kagwe ameongezea kwamba wagonjwa waliofariki wanatoka miji ya Nairobi na Mombasa.
 
Waziri huyo pia amepiga marufuku usafiri wa Wakenya kuelekea katika maeneo ya mashambani akionya kwamba huenda wakapeleka maambukizi ya virusi hivyo katika maeneo hayo.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE 

No comments:

Post a Comment