Breaking

Tuesday, April 21, 2020

Wabunge Wataka Wapimwe Corona ili Kuondoa Hofu Waliyokuwa Nayo


Mbunge wa Tarime vijijini (Chadema), John Heche na Mbunge wa Bunda Mjiji (Chadema), Ester Bulaya, wametaka wabunge wote kupimwa ugonjwa wa Corona ili kuondoka hofu.

Heche amesema Naibu Spika ametangaza mmoja wao bungeni amethibitika kuwa na Corona.

“Maombi yangu wizara itupime wote hapa bungeni kujua hali halisi,” amesema Heche katika ukurasa wake wa Twitter.

“Getini tunapita pamoja na ukaguzi na hata canteen. Busara ni wote tupimwe kuondoa hofu,” aliandika Heche
Mbunge Bulaya amesema mara ya kwanza waliomba wabunge wapimwe saivi imekuwa ni shida. “Tulishauri wananchi wapimwe hatukusikilizwa hivi tutamlaumu nani, serikali acheni kiburi watu wanakufa, wagonjwa wanaongezela,’
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment