Breaking

Tuesday, April 14, 2020

Watu 8 Wafariki kwa Kusombwa na maji Manyara

Vifo vya watu waliofariki kwa kosombwa na maji wilayani Kiteto mkoani Manyara, vimefika nane kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo.


Mvua hizo zimesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu na mazao mashambani na kupelekea kutishia uhai wa binadamu.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magesa amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo, wakati akiwa katika zoezi la kuokoa mwili wa mwananchi mmoja aliyefariki kwa kusombwa na maji katika daraja la Chem chem.

Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi kuchukua tahadhari pindi wanapovuka sehemu zenye maji mengi hasa katika kipindi hiki cha mvua nyingi.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment