Breaking

Sunday, April 26, 2020

Zambia yapiga Stop Magari Kutoka Tanzania Sababu ya Corona, Zitto Amsihi Rais Magufuli Alipe uzitoSerikali ya Zambia imepiga marufuku mwingiliano wa kibiashara nan chi ya Tanzania hatua ambayo Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo na Mbunge wa Jimbo la Kigoma mjini Zitto Kabwe amesema inapaswa kumstua Rais John Magufuli.


Taarifa ya Jimbo la Zambia lililopo mpakani mwa Tanzania ambayo imeenea katika mitandao ya kijamii imeeleza kuwa marufuku hiyo inazilenga hasa magari mapya yanatokea bandari ya Dar es Salaam maarufu kama IT.

“Nchi yetu sasa ni tatizo kwa majirani. Serikali ya Zambia imeanza kuweka KUFULI kwa magari kutoka Tanzania. Wanatekeleza maamuzi ya nchi za Sadc Bahati mbaya sana nchi yenye uenyekiti wa SADC ndio sasa inaonekana tatizo. Namsihi Rais John Magufuli achukulie kwa uzito jambo hilo”

Zitto ameandika hayo katika ukurasa wake wa Twitter akiambatanisha barua hiyo kutoka Zambia ambayo inaonyesha kuwa hatua hiyo ya marufuku imechagizwa na kuongezeka kwa visa vya Corona nchini

Nchi yetu sasa ni tatizo kwa majirani. Serikali ya Zambia imeanza kuweka KUFULI kwa magari kutoka Tanzania. Wanatekeleza maamuzi ya nchi za @SADC_News. Bahati mbaya sana nchi yenye uenyekiti wa SADC ndio sasa inaonekana tatizo. Namsihi Rais @MagufuliJP achukulie uzito

View image on Twitter

111 people are talking about this

No comments:

Post a Comment