Breaking

Saturday, April 18, 2020

Zuchu Ataja Siku ya Kumuanika Mpenzi Wake....


Msanii mpya ndani ya WCB, Zuchu amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hayopo kwenye mahusiano yoyote ya kimapenzi na siku ya ndoa ndipo watu watamjua mpenzi wake.

Zuchu ambaye jina lake halisi ni Zuhura, ameeleza hayo kwenye mahojiano na kipindi cha The Switch cha #WasafiFM ambapo amesema amemua kutokuwa kwenye mahusiano kufuatia ushauri wa Queen Darleen.

“Kwa sasa sipo katika mahusiano yoyote ya kimapenzi, ni ushauri wa dada yangu Queen Darleen nimeupokea vizuri Sana, mpaka ifike siku ya ndoa ndio mtamjua mpenzi wangu rasmi ” amesema Zuchu.

Katika hatua nyingine amesema kuwa #Mbosso ni msanii wa WCB ambae alikua anamtia moyo sana, siku zote alikuwa anamsisitiza hatakiwi kukata tamaa.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment