Breaking

Wednesday, May 13, 2020

Baada Ya Siku 57 Mtoto Wa Mbowe Apona Corona


Mtoto wa Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema), Dudley Mbowe, ametangaza kupona rasmi virusi vya Corona ikiwa ni baada ya kupatiwa matibabu kwa takribani siku 57.

Dudley ametangaza taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter huku akishukuru watoa huduma wa hospitali ya Temeke alikokuwa akipatiwa matibabu.

“Baada ya siku 57 hatimaye nimekutwa sina maambukizi..Shukrani na heshima kubwa madaktari na wauguzi wa hospitali ya Temeke hawa ni nyota wa mchezo ” ameandika

Ikumbukwe kuwa Dudley alikuwa mmoja kati ya watu wa mwanzoni kabisa kukutwa na virusi vya corona nchini.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment