Breaking

Sunday, May 10, 2020

Bilionea Mo Awajibu Wanaomshinikiza Kutoa Msaada Mapambano ya Corona, Asema Kutoa ni Moyo si Utajiri


Bilionea maarufu nchini Tanzania Mohammed Dewji amewajibu wale wanaotaka kutoa msaada wa kibinadamu kama wanavyofanya Matajiri wengine wakati wa janga hili la ugonjwa corona.

Watu wengi wamekuwa wakiibuka katika ukurasa wa mitandao ya kijamii ya Tajiri huyo kijana Afrika katika kila posti wakimtaka naye kuiga mfano wa matajiri wengine kutoa msaada kusaidia mpambano dhidi ya corona.

Kupitia mtandao wa twitter Mo amesema kutoa ni moyo na si utajiri. Jambo ambalo limetafriwa kama majibu kwa wanomshinikiza kutoa mchango.

Masaa mawili baada ya posti hiyo ya kwanza Mo aliandika tena kuwa Kuna vingi vya kumuomba Mungu kabla ya kumuomba utajiri.

Hata hivyo Mo amekuwa wakihamasisha watu kuchukua tahadhari kujilinda na ugonjwa huo ambao umekuwa tishio kwa nchi nyingi duniani.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment