Kiungo huyo hivi karibuni alikuwa akitajwa kuwaniwa vikali na Yanga ambayo inaelezwa alitengewa dau la Sh Mil 80 ili asaini mkataba wa miaka miwili ya kukipiga Jangwani.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Dilunga alisema kuwa ndoto zake zimefanikiwa za yeye kucheza kwenye klabu kubwa hapa nchini za Simba na Yanga, alichobakisha yeye ni kucheza nje ya nchi.
“Ndoto za wachezaji wengi hapa nchini ni kucheza klabu kubwa za Simba na Yanga ambazo mimi pia ilikuwa ndoto zangu ambazo zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwangu.
“Nimepata taarifa za mimi kutakiwa na timu yangu ya zamani ya Yanga, nilikuwa tayari kurejea huko lakini kwa hivi sasa sitakuwa katika sehemu nzuri ya kurejea huko.
“Ninataka kutimiza malengo yangu ya mimi kucheza nje ya nchi na huu ninaamini ndiyo wakati wangu muafaka wa kwenda huko kucheza kama siyo nchi za Ulaya basi Afrika,” alisema Dilunga.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE
No comments:
Post a Comment