Breaking

Sunday, May 10, 2020

Fei Toto Akubali Kutua SIMBA SC Kwa Masharti


Feisal Salum, 'Fei Toto' kiungo anayekipiga ndani ya Yanga ambaye miongoni mwa viungo anaowakubali ni pamoja na Clatous Chama anayekipiga ndani ya Simba ameonesha nia yabkuibukia huko kwa masharti.

Kiungo huyo amesema kuwa anaweza kucheza ndani ya Klabu ya Simba iwapo viongozi wake watamruhusu kufanya hivyo.

"Bado nina mkataba mrefu na Yanga kwa sasa lakini sina shida iwapo inatokea Klabu ya Simba ama Klabu nyingine zikahitaji saini yangu nitafanya nikiwa ruhusa.

"Mimi ni mchezaji wa Yanga viongozi wananipenda nami nawapenda pia ikitokea klabu inahitaji saini yangu utaratibu ufuatwe sina hiyana nitasaini bila tatizo," amesema.

Fei Toto yupo zake Visiwani Zanzibar kwa sasa baada ya ligi kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment