Breaking

Saturday, May 16, 2020

Harmonize Amuomba Msamaha Mkewe "Nina Ndoto Kubwa Nataka Nitimize"

Msanii na mmiliki wa lebo ya Konde Music Worldwide 'Harmonize' amelazimika kumuomba msamaha mke wake Sarah kutokana na kutomuelewa hasa kwenye masuala ya kazi.

Harmonize amesema hayo kwenye Friday Night Live (FNL) ambapo amesema kuwa mara nyingi mke wake amekuwa hamuelewi ni kwanini hatumii muda mwingi kuwa naye, akisema kuwa ni kwa sababu ya kazi.

"Napenda kumshukuru Mungu kwa baraka zake, Management yangu na wazazi wangu lakini pia mke wangu anisamehe kwa kumsahau, yeye ni mtu wa muhimu sana kwangu", amesema Harmonize.

"Muda mwingine amekuwa akinilalamikia kwanini narudi usiku sana nalala na naamka saa nne nimemuacha amelala ninaenda kazini, kwahiyo tumepitia sana changamoto hizo lakini nitumie nafasi hii kumuomba msamaha, nimampenda sana mke wangu. Ninafanya hivi kwa sababu nina ndoto kubwa nataka niitimize", ameongeza.

Harmonize hivi sasa anaitangaza albamu yake ya 'Afro East' pamoja na Extended Playlist (EP) ya msanii wake Ibraah inayoitwa 'One Step' ambayo ina ngoma tano.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment