Breaking

Thursday, May 14, 2020

Hatimaye Haji Manara Aamua Kuwa Mkweli...."Nimeachana na Mke Wangu Kaolewa na Mwanaume Mwingine"

Msemaji wa Simba, Haji Manara hatimaye amekiri kuwa ameachana na mkewe na tayari mwanamke huyo amekishaolewa na mtu mwengine .

Manara amesema alilazimika kufanya hivyo kutokana na presha kubwa kutoka upande wa mke wake.

Amesema kulikuwa kuna presha kubwa sana upande mke wake hadi akafikia kuamua kuachana naye. “Siku chache baadaye nikasikia ameolewa, wala sikushituka kwa kuwa hili nilijua lilikuwa limeandaliwa na linakwenda kuwa hivi,”

Aliongeza kwa kusema kuwa “Kwa sasa nasubiri kwanza lakini nitaoa na mwanamke ninayetaka kumuoa lazima awe mrembo sana. Nataka mwanamke mrembo hasa, suala la tabia litafuatia.”

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment