Breaking

Saturday, May 2, 2020

Historia Ya Kaburi la Ajabu Mkoani Iringa Lililogoma Kuhama ' Maiti yake Ilizikwa na Mtu Akiwa Hai"


Kaburi la Mzee Martin Kiyeyeu aliyefariki mwaka 1974, kama linavyoonekana katika picha kando ya barabara ya Iringa-Mbeya

uliwahi kusikia maajabu ya Kaburi hili la mtu maarufu katika fani ya waganga wa jadi Almaarufu Kiyeyeu?

NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO BONYEZA HAPA

Kaburi la Kiyeyeu, lipo Njiapanda ya Mlolo pembezoni kabisa mwa barabara iendayo Mkoani Mbeya ukitokea Iringa lipo upande wako wa kulia, katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Hili ni kaburi alilozikwa mtu mmoja aliyekuwa Mganga maarufu wa jadi katika ukanda mzima wa maeneo ya mkoa huo, ambaye alifariki dunia miaka ya nyuma kidogo lakini hadi leo hii kaburi hilo ukiliona ni kama limejengwa jana.  Ukiangalia kwa makini picha hii utaweza kuona jinsi nyaya za umeme wa Tanesco zilivyokwepa kaburi la Martin Kiyeyeu

Baada ya kufariki dunia mganga huyu, alizikwa kwa kufuata taratibu na mira za Machifu ambapo alizikwa kwa kusindikizwa na mtu aliye hai, aliyejitolea kwa ajili ya kuzikwa naye akiwa hai ili kumsindikiza, ambapo inadaiwa mtu huyo aliketi na kumpakata mganga huyo aliyezikwa huku akiwa amekaa.


Kaburi hilo limekuwa liwashangaza watu waliowengi na hata ndugu wa marehemu huyo kutokana na kuwa na maajabu na miujiza isiyoisha kana kwamba mtu huyo amezikwa mahala hapo jana.
Moja kati ya maajabu makubwa yaliyowahi kutokea mahala lilipo kaburi hilo ni wakati Shirika la umeme lilipokuwa katika zoezi la kuweka Nguzo za umeme pembezoni mwa barabara hiyo na kutokana na kaburi hilo kuwa karibu kabisa na barabara kubwa.  Ndipo ilipoamuliwa kuweka nguzo hizo na kupitisha nyaya za umeme kiubishi.Lakini baada ya kumaliza zoezi hilo walishangazwa kwa kuona kuwa eneo la juu ya kaburi hilo hapakuwa ukipita umeme hali ya kuwa ulipoanzia hadi kabla na baada ya kaburi hilo umeme umejaa tele, ila eneo la juu ya kaburi hilo tu hakuna umeme.

Jambo hilo liliwafanya Tanesco kukubali matokeo na kuamua kuchukua uamuzi wa busara kwa kuhamishia baadhi ya nguzo hizo upande wa pili wa barabara ili kukwepa eneo hilo, hivyo nyaya hizo zikavuka barabara kabla ya kufikia kaburi hilo.

Baada ya kulivuka kaburi hili, na baada ya kufanya hivyo ummeme huo uliwaka na hadi hii leo unaendelea kuwaka, hivyo Serikali japo haiamini uchawi lakini hapa iliamini uchawi upo.

Moja ya maajabu ya kaburi hilo ni kushindwa kupitishwa kwa umeme kupita juu ya yake na pia linadaiwa kushindikana kuondolewa mara mbili na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo aliyeuawa kwa nyuki na mwingine kufariki ghafla akiendesha tingatinga alipokuwa akijaribu kuling’oa.

Hata hivyo kaburi hilo na mengine 21 yaliyokuwa kwenye eneo hilo yaliondolewa na kuhamishiwa upande wa pili wa barabara, ambako kulikuwa na kaburi moja la mtoto wa kike wa Kiyeyeu, ambaye hakuzikwa katika eneo lililokuwa na makaburi ya ndugu zake baada ya mila na matambiko kufanyika.

NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO BONYEZA HAPA

Unaweza Kusikiliza Simulizi ya Hadithi hiyo hapa Chini:


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

1 comment: