Breaking

Friday, May 15, 2020

Hotuba ya Chedama yakataliwa Bungeni kisa aliyeiandika, masharti

Spika wa Bunge Job Ndugai ametoa sababu za kutoruhusu hotuba ya upinzani kusomwa Bungeni akisema imeandaliwa na mtu ambaye haruhusiwi kuingia Bungeni.

Amesema mwandishi wa Hotuba hiyo (Halima Mdee) ni miongoni mwa ambao hawatuhusiwi kuingia bungeni haiwezekani hotuba yake ipitishwe dirishani.

Masharti yaliyotolewa na Spika Ndugai kwa wabunge wa Chadema baada ya kutangaza wiki mbili za kutoingia bungeni ni kurudisha posho walizopewa na kuwasilisha vipimo kuwa hawana ugonjwa huo.

Aidha Leo Mei 15 Wizara ya fedha ilikuwa ikiwasilisha hotuba ya bajiti yake ya mwaka wa fedha 2020/2021 ambapo kambi rasmi ya upinzani bungeni ilipaswa nayo kuwasilisha hotuba yake.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment