Breaking

Wednesday, May 20, 2020

Ibraah wa Harmonize Aeleza Alivyosafa Miezi Miwili Getini

EATV & EA Radio Digital, imepiga stori na msanii wa Konde Music Ibraah Tz, ambaye yupo chini ya Harmonize, na amesema kabla hajatoka alihangaika sana kumpata Harmonize ila aliishia getini kwa miezi miwili na hakumpata.


Ibraah Tz amesema anamshukuru Harmonize kwa sababu, alimkuta hayupo vizuri na bila ya kuwa na kipaji cha kutosheleza lakini akatengenezwa hadi amefikia alipo sasa.

"Kabla ya hapo nilikuwa naendaga sana getini kwake kuomba nafasi ya kuonana naye na nikafanya hivyo kwa miezi miwili lakini sikupata nafasi hiyo, ila kuna mjomba wangu alikuwa ananisadia kunipa nauli, akajitahidi kunikutanisha na producer Bonga ndiyo nikapata nafasi ya kufika Konde Music" ameeleza Ibraah Tz

Pia Ibraah Tz ameendelea kusema kabla hajasainiwa Konde Music, ameshazunguka sana kwenye studio na wasanii wengine kutafuta msaada ila ikashindikana japo hawezi kuwazungumzia kwa sasa wasanii hao ni kina nani.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment