Idadi ya vifo vinavyotokea ya kila siku imeongezeka kwa wastani hadi 2000 tangu katikati ya mwezi wa Aprili, licha ya hatua zinazotekelezwa kumaliza janga hilo.
Idadi hii iko juu zaidi ya ile ya homa ya msimu kwa miaka yote tangu mwaka 1967, pia inazidi ile ya UKIMWI kwa kipindi cha miaka ya 1981 hadi 1992, ikimaanisha miaka kumi na moja kufuatia kuanza kwa ugonjwa huo.
Kuhusu idadi ya visa vya maambukizi, zaidi ya watu milioni 1.3 wamepata virusi vya Corona na idadi ya jumla ya kila siku inaendelea kuongezeka, hasa huko Mississippi, Minnesota na Nebraska.
Kwa upande mwingine, idadi ya maambukizi imepunguka katika jimbo la New Jersey na Jimbo la New York
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE
No comments:
Post a Comment