Breaking

Thursday, May 14, 2020

Kigogo wa Chadema Ahoji Ukimya Ripoti ya kamati ya Waziri iliyochunguza Maabara ya Kupima Corona

Wabunge Chadema walazwa Aga Khan, polisi wakanusha kuwapiga ...Mkurugenzi wa Mawasiliano na mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema John Mrema amahoji ukimya katika ripoti ya kamati ya Waziri wa afya Ummy mwalimu ya kuchunguza ofisi ya maabala ya taifa ya afya ya jamii.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter Mrema amesema amehoji akisema “Leo ni tarehe 13 Mei, 2020 hii kamati ya uchunguzi wa Maabara ya Taifa ilipaswa iwe imeshawasilisha tarifa yake ya uchunguzi. Mbona kimya? Au ripoti imekuwa tofauti na Hadidu rejea?”

Itakumbukwa kuwa Mei 4, Waziri wa afya Ummy Mwalimu aliwasimamisha kazi Mkurugenzi wa maabara ya taifa ya afya ya jamii Dk Nyambura Moremi na Meneja udhibiti ubora wa Jacob Lusekelo ili kupisha uchunguzi kufuatia kauli ya Rais John Magufuli Mei.

Katika hotuba yake Rais John Magufuli baada ya kumuapisha waziri Mpya wa katiba na sheria alisema kuna warakini katika vipimo vya Covid-19 nchini akisema ofisi yake ilipeleka sampuli ya vitu mbalimbali ikiwemo papai, fenesi, oili, mbuzi na kondoo babdo vimo vikatoa majibu na kati ya vitu hivyo kuna vilivyokutwa na ugonjwa wa corona.

Pamoja na hatua hiyo Waziri Ummy aliunda kamati ya watalaam 9 ikiongozwa na Profesa Eligius Lyamuya wa Chuo kikuu cha Muhas ili kufanya uchunguzi wa mwenendo wa baabara ya taifa ya jamii ikiwemo mfumo mzima wa ukusanyaji wa sampuli za ugonjwa wa corona (Covid-19) ambayo ilitakiwa kuwasilisha tripoti kwake kabla ya Mei 13, 2020.
 HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment