Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Papamafido ametumia kodi ya nyumba na kulazimika kulala nje baada ya pesa hiyo kwenda kuchorea ‘TATTOO’ ya Wema Sepetu.
Papamafido ambaye hapo jana alibahatika kuonana uso kwa uso na Wema, alishindwa kuzuia hisia zake na kuvua shati lake alilovaa kisha kumuonyesha Wema Sepetu ‘Tattoo’ kubwa yenye sura yake aliyoichora nyuma ya mgongo na kumuacha Msanii huyo akishika mdomo pasipo kuamini mapenzi makubwa aliyoonyesha kijana huyo.
Mbali na kujichora huko ‘Tattoo’ iliyopelekea hadi baadhi ya ndugu zake kumtenga huku marafiki zake wa karibu kumcheka, lakini pia alikuwa na michoro mingine ambayo amemchora Wema Sepetu katika vibao na kumkabidhi.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE
No comments:
Post a Comment