Breaking

Friday, May 15, 2020

Kilewo "Tumemtafuta Mchome Vituo vya Polisi Dar Mpaka Sasa Hatujampata"


Wakili Henry Kilewo amesema jana walipatiwa taarifa kuwa Katibu wa Chadema Wilaya ya Mwanga, Lembrus Mchome, amesafirishwa na jeshi la polisi kutoka mkoani huko kuelekea Dar es Salaam.

“Mpaka ninapoandika hapa tumepita kwenye vituo kadhaa vya police hapa DSM bila kumuona,” aliandika Kilewo kwenye ukurasa wake wa twitter.

Mchome alikamatwa Mei 11, 2020 akiwa Wilaya Mwanga akituhumiwa  kupiga picha gari ya bosi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Jana zilisambaa taarifa ya kuwa Mchome anasafirishwa na jeshi la polisi kutoka Kilimanjaro kwenda mkoa wa Dar es Salaam.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment