Breaking

Saturday, May 2, 2020

Kim Jong-un Aonekana Hadharani, Afanya Hili Kukiwa na Tetesi Kuwa Amefariki


Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Habari la nchi hiyo ‘KCNA’ leo, Mei 2, 2020, wakati ambapo kuna uvumi kuwa huenda alikuwa mahututi au amefariki dunia.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Kim amekata utepe na kufungua kiwanda kikubwa cha mbolea katika mji mkuu wa chi hiyo, Pyongyang, tukio lililofanyika Ijumaa, Mei Mosi, 2020.

KCNA imeripoti kuwa tukio hilo lilihudhuriwa na watu wengi ambao waliitikia kwa shangwe kuu baada ya kiongozi huyo kukata utepe kuashiria kufunguliwa kwa kiwanda hicho.

Imeelezwa kuwa aliongozana na maafisa waandamizi wa serikali akiwemo mdogo wake, Kim Yo Jong.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment