Breaking

Tuesday, May 19, 2020

Kisa Mpiga Picha wa Diamond Platnumz...Khaligraph Jones Awaonya Mbosso na Lava Lava "Chungeni Sana Ama Niwafagilie Nyinyi Wote!”

Inaonekana msanii Mbosso na Lavalava hawajui vile rapa Khaligraph Jones hufanya kazi yake ya muziki. Kwa muda alimnyamazisha msanii wa nchi ya Nigeria kwa kuwashauri mashabiki wake wamtanie.

Haya basi inaonekana kuna ugomvi kati ya OG na familia ya lebo ya Wasafi baada ya khaligraph kudai kuwa mpiga picha wa lebo hiyo alikataa kumtumia picha zake.


Katika mitandao ya kijamii, mpiga picha Lukamba aliposti ujumbe wa kijinga, lakini hakujua kuwa alikuwa anacheza na moto wa kuotea mbali.

Katika posti hiyo, Lavalava aliandika maoni yake na kisha Mbosso hakuachwa nyuma naye alikuwa na haya ya kusema;

“Dah Sijafikia huku ..Changamoto za card zinataka kunigombanisha na Kaka yangu OG @khaligraph_jones Bro siku Tukikutana yaani nakupiga album mzima na kupa hapo hapo 🤣 #respecttheogs.” Aliandika Mbosso.

Alipoona vile wasanii hao hawakuwa na heshima aliamua kuwapa bonge la jibu huku mashabiki wakiwaambia Mbosso na Lavlava wasicheze na mkuu wa wakosoaji.


“@Lavalava @Mbosso naona mumechekeshwa sana. Lakini huyu kijana wenyu nyinyi wote murudi ushago. Chungeni sana ama niwafagilie nyinyi wote kama Mr Nice. You will respect the OG.” Aliandika Khaligraph Jones.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment