Breaking

Saturday, May 9, 2020

Kisa Shiti, Rachel Povu Kama Lote

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Winifrida Joseph ‘Rachel’ amewatolea povu baadhi ya mashabiki wanaokomenti shiti kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na Amani, Rachel amesema amekuwa akisikitishwa na komenti za aina hiyo ambazo zinawekwa lango la kuwavunjia hadhi wasanii.

“Hakuna kitu ambacho kinaniboa kama mashabiki kuwakomentia wasanii vibaya.

“Yaani unakuta msanii anaweka picha nzuri kwenye ukurasa wake wa Instagram, kwa mfano akiwa amevaa vizuri, lakini ‘mijitu’ inakuja kukomenti ovyo.

“Ukifuatilia mtu anayemponda msanii, hana hata uwezo wa kunua nguo au kufika hadhi ya msanii anayemdharau,” alisema Rachel.

Stori: Khadija Bakar

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment