Breaking

Friday, May 1, 2020

Kusepa Kwa Jonijo Wasafi; Je, Lil Ommy Anachangia?

Ni muda kipindi cha Block 89, mimi hukiita kipindi mama cha Wasafi FM, yeah its true ndio kilichoanza, hakiruki hewani.
Kuanzishwa kwa kipindi kipya cha The switch kulipelekea kipindi hiko kisiruke kwa sababu Maudhui yanafanana, nilishaleta uzi humu.

Kulikuwa na majadiliano kabla ya The Switch kuanza? Well, mazungumzo yalikuwepo ila muafaka haukufikia ndio maana kipindi kikasimama na The Switch ikachanja mbuga japo naona ni kipindi cha kawaida na siku zinavozidi kwenda ni kama The Playlist version 2 na Lil Ommy ndio ana dominate kipindi huku co-host Ray Mshana na Ammy Gal ni kama wasindikizaji.

Je, Lil Ommy hawaelewani na Jonijo tangu Times FM? Kuna tetesi kuwa walikuwa hawaivi tangu Times FM, na jamaa Lil Ommy ilikuwa kama ka dominate pale, japo Lil Ommy huwa hakubali hilo, pia huwa haelezi ukweli kama alimuonesha tobo Jonijo la Wasafi, japo wadau wanadai Jonijo alipewa mchongo na Ommy wa kusepa Wasafi.

Baadae wanakutana wote Usafini, na Jonijo anatakiwa adrop kwenye Block 89, abaki kwenye Bartender huku Brand iliomuweka mjini ya "Now you Know" ikipotea ambayo wengi walimjulia huko, ni kama ilimkata ila no way out.

Makubaliano ya kukifuta au kukibadili ratiba kipindi cha Block89 kama hakukubaliana nayo na kukaa pembeni hiyo inampa nafasi Lil Ommy kuteka waves za Usafini na jamaa kukaa bench pamona na wenzake wa2 ambao haileweki wanaelekea wapi.

Baadae tunaona Majizo kalamba Dume huku Wasafi wakipoteza mashabiki wa Jonijoo kwenye Bar tender na Block89, Jonijoo kaenda Efm, je atatangaza kipindi gani redion au Kwenye Tv? Namuona Jonijoo akisettle pale na kufanya makubwa zaidi ya alipokuwa awali.

Bila Lil Ommy kwenda Wasafi Jonijoo angeendelea kuwepo na kushine kupitia Bartender. Kutoelewana na Lil Ommy, shida ilishawahi tokea pia kwa Calipso kipindi yupo Timesfm kwenye Playlist iliomekana kama jamaa anambania na akasepa Clasaic fm, maneno yakaja kijiweni kua Ommary ni mtu sio na kile kipindi hataki mtu mwingine, swali Ammy gal kawezaje mpaka wamefika hapa?

Me sijui, Baada ya Lil Ommy kufika Wasafi hao hao pia wanatandika daruga.

Yetu macho Ya Kuku Mayai aacha mchezo Uendelee

Tchaoo

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment