Breaking

Sunday, May 10, 2020

Lema ahoji kurejeshwa kwa Mwambe bunge asema ni ukiukwaji wa sheria

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amehoji kitendo cha kurejeshwa bungeni aliyekuwa Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe, ambaye alitangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) hadharani.

“Cecil Mwambe amerudi kuendelea kuwa mbunge hata baada ya kujiunga na CCM hadharani?. This is more than impunity,” aliandika Lema katika ukurasa wake wa Twitter.

Aliongezea kuwa ” Hakuna tena sheria? Nchi imeharibika mbele ya macho yetu! Idara ya usalama wa taifa inafanya kitu gani na kushauri nini?,” aluhoji Lema

Lema amesema kitendo hicho ni uasi mkubwa dhidi ya utawala wa sheria.

Jana Mwambe alitinga bungeni baada ya Spika wa Bunge kumuambia arejeshee na kuendekea na shughuli za bunge.

Baadhi ya wadau walikuwa wakihoji Mwambe atakuwa ni mbunge wa chama gani bungeni licha ya kujiudhuru na kuhamia CCM.

Mwambe amesema kuwa kwa sasa amerejea Bungeni rasmi kumalizia muda wake wa Ubunge kwa kipindi kilichobaki na kwamba yeye ni mwanachama halali wa CCM, hivyo uchaguzi ujao atagombea kupitia tiketi ya CCM.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment