Breaking

Wednesday, May 20, 2020

Magufuli Ateta Na Kenyatta Mipaka Kufunguliwa

Details of President Uhuru Kenyatta's private visit to Tanzanian ...Rais John Magufuli amesema kuwa amezungumza na rais wa Kenya Uhuru Kenyata na kukubariana kutatua migogoro iliyoibuka kwenye sehemu  mipaka baina ya nchi hizo mbili na kwa kuwakutanisha wakuu wa mikoa ya mipakana pamoja na mawaziri wa uchukuzi wa nchi zote mbili

Akizungumza na wananchi wa Singida leo akiwa anaeleka mkoani Dodoma Rais Magufuli amesema haiwezekani kila dereva anayepimwa mpakani akutwe na virus vya Corona

“Juzi nikiwa Chato alinipigia simu rais wa Kenyatta na tukaongea juu ya swala la mgogoro kule mpakani tumekubaliana kuwa wakuu wa mikoa ya mipakani kati ya Kenya na Tanzania kukutana na kutatua tatizo hili haraka iwezekanavyo ili biashara ziendelee kufanyika baina yetu” amesema

“Mawaziri wa uchukuzi wa kenya na watanzania na makatibu wakuu wa wizara ya mambo ya nje watengeneze utaratibu ndani ya wiki hii wakutabe hili jambo liweze kuisha haraka tunataka vituunhguu vya hapa Singida viuzwe kenya na sabuni za kenya ziuezwe hapa “ ameongeza

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment