Breaking

Friday, May 1, 2020

Marioo "Nipo Single Miaka yote Bado Sijapata Mpenzi"


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Marioo, amefunguka kusema kuwa yupo single kwenye maisha yake yote kwa sababu bado hajapata mtu anayemtaka.


Akitaja vigezo anavyovitaka ili kumpata mwanamke anayemfaa msanii huyo amesema, lazima awe mzuri ili hata akipita naye sehemu watu wamuogope na anachopenda zaidi kwa mwanamke ni maumbile "umbo".

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital Marioo amesema  "Mimi binafsi nipo single miaka yote kama batani ya suti, kuwa kwenye mahusiano au kutokuwa ni maamuzi ya mtu mwenyewe na sidhani kama kuna sababu ya mimi kuwa single, nimeamua tu"

"Nipo single kwa sababu sijapata mtoto ambaye ninamtaka, kama kuna mtu yeyote anakaribishwa ila vigezo na masharti ya kuwa naye lazima awe mzuri, hata nikipita naye watu waogope, kwa mwanamke naanza kupenda umbo lake kwanza jinsi alivyo halafu masuala ya tabia nitazijua baadaye".

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment