Breaking

Thursday, May 7, 2020

Mbunge Sugu amesema yupo Dar anakunywa supu ya Pweza, Bashite ni kichekesho


Mbunge wa Mbeya Mjiji (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu amesema yupo Dar es Salaam na anapata supu ya pweza , Bashite ni kama kichekesho tu.

Sugu aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter kuwa “Niko zangu Dar napata supu ya pweza Bashite is just a Clown,”.

Jana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alitoa saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es salaam “kula bata” kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo watakamatwa kwa kosa la kuzurura kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura usiku.

Makonda amesema mbunge anaepaswa kuwa Dar es salaam ni yule mwenye Kibali au ruhusa ya Spika wa Bunge tofauti na hapo ni vyema wakafunga virago vyao na kurudi bungeni ili kuepuka kukamatwa.

“Hakuna asiyefahamu kuwa sasa hivi tuko katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona na sio uzururaji, ifahamike huu sio mji wa wazururaji hivyo natoa saa 24 kwa wabunge wote kurudi Dodoma tofauti na hapo tutawakamata kwa kosa la uzururaji kama tunavyowakamata Machangudoa” alisema  Makonda.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment