Breaking

Wednesday, May 20, 2020

Msanii 20% Afunguka Stori ya Neema na Kupata Watoto WengiMsanii wa BongoFleva aliyetamba kipindi cha nyuma 20 Percent, amefunguka kusema ile filamu yake ya 20% Furaha Iko Wapi na wimbo wa Mama Neema, ni stori ya kweli japo haimuhusu moja kwa moja.

Akipiga stori na Big Chawa kwenye kipindi cha PlanetBongo ya East Africa Radio, msanii huyo ameeleza kuwa,  "Ile ngoma ya Mama Neema ni stori ya ukweli japo hainuhusu mimi moja kwa moja na ilitoka mwaka 2007, Neema sasa hivi ni mkubwa na anajiheshimu pia anasifa kama za Monalisa japo kwa sasa yupo nchini Rwanda, halafu binafsi nimebarikiwa kupata watoto wa kutosha yaani ninao wengi" amesema  20 Percent.

"Nakuja na filamu ya pili ya Mama Neema, itaonesha Neema alivyotoroshwa na mama yake mdogo kwenda Rwanda, kipindi naiachia ile filamu zilivumishwa stori eti nilikataza nyimbo zangu zisipigwe kwenye Media, ndiyo maana nikazihamishia kwenye ile filamu" ameongeza.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment