Breaking

Saturday, May 2, 2020

Mwalimu Jela Miaka 30, viboko 30 kwa Kubaka Mwanafunzi


Mahakama ya wilaya ya Ileje mkoni Songwe imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela na kuchapwa viboko 30 Abeid Rajabu Mbuba(54) amabye ni mwalimu wa shule ya msingi Shinji kata ya Mbeba.

Hakimu Shughuli Mwampashi ametoa hukumu hiyo baada ya kusikiliza pandezote mbili na kuridhika na ushahidi upande wa Mashtaka na kumuhukumu mtuhumiwa kutumikia kifungo cha mika 30 jela na kucharazwa fimbo 30 ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.

Awali mwendesha mashtaka Peter Mrisho aliomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa kwani vitendo vya ubakaji vimekithiri wilaya ya Ileje ambapo hukatishandoto za wanafunzi kwa kuwapa mimba.

Hata hivyo Hakimu Mwampashi alitafakari ombi hilo na kuamuru akatumikie kifungo cha mika 30 jela na kuchapwa viboko.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment