Breaking

Saturday, May 23, 2020

Mwigizaji ROSA Ndauka Ajitetea Kuolewa Ndoa ya Kiislamu...."Nilikuwa Napenda Kwenda Kanisa"

Mwigizaji ROSA Ndauka Ajitetea Kuolewa Ndoa ya Kiislamu...."Nilikuwa Napenda Kwenda Kanisa"
Msanii wa filamu Rosse Ndauka amesema, amekuwa katika Dini na malezi ya Kiislamu tangu zamani kwa sababu mama yake ni mtu wa Dini hiyo ila baba yake ndiyo alikuwa Mkristo na kumfuata yeye.


Rosse Ndauka amesema hayo kwenye show ya Dadaz ya East Africa TV, ambapo ameulizwa kuhusu kubadili Dini baada ya kuolewa na mwanaume wa Kiislam aitwaye Haffiyy.

"Mimi ni Muislam tangu utotoni, mama yangu Muislam na nimekulia katika malezi ya Uislam, japo Baba yangu ni Mkristo na nilikuwa napenda kwenda kanisani, ila baada ya kuwa na mume Muislam nikatoka kwenye Ukristo kuingia kwenye Uislam" amesema.

Msanii huyo wa filamu  ameendelea kusema  "Upendo ndiyo kila kitu na namshukuru Mume wangu anaupendo sana, hata baba wa huyu mtoto wangu sikuachana nae kwa ubaya na nilipoingia kwenye ndoa alinitumia ujumbe wa kunipongeza".

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment