Breaking

Sunday, May 3, 2020

Ndugai Adai Mbowe Anaamrisha Wenzake Kama watoto


Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema kuwa kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, haimbabaishi na chochote kwa kuwa kila jambo lao wanaweka upinzani na Wabunge ni timu moja na yeye ameamrisha timu yake tu bila kushirikisha wenzake, hivyo Wabunge wa CCM watabaki  na kuendeshesha Bunge.


Spika Ndugai ameyabainisha hayo leo Mei 2, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kuongeza kuwa agizo la Mbowe kwa Wabunge wake wamelipokea kwa mikono miwili, na kwamba amekuwa ni kiongozi wa kuamrisha tu na ndiyo maana wanachama wake wengi wanahama, na kuongeza kuwa janga la Corona ni la Dunia nzima na hakuna ambaye anapenda kuona watu wakifa.

"Sisi halitushangazi hawa wenzetu kila jambo lazima waweke upinzani hata kama ni janga, Wabunge ni timu moja hauwezi kuamrisha tu wachezaji wako kwamba tokeni bila kuzungumza na wenzako, Wabunge wa CHADEMA wana bahati mbaya sana kazi yao ni kuamrishwa tu kama watoto wa Primary vile na wanalalamika kimya kimya sana kwangu" amesema Spika Ndugai.

Aidha Spika Ndugai alizungumzia suala la kupokea ushauri wa Mbowe "Wala siko tayari tena, yeye aendelee tu na Methodology zake kwa sababu muda mfupi ujao tutamaliza Bunge kwa kuzingatia tatizo la Corona na toka tumeanza tumezingatia na tumebadilisha mambo mengi sana".

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment