Breaking

Sunday, May 3, 2020

Official Nai Aruka Kiunzi...Akanusha Kuolewa

BAADA ya kudaiwa kuwa amefunga ndoa ya kimyakimya, video vixen Bongo, Official Nai ameibuka na kufafanua ukweli wa mambo.


Akizungumza na Mikito Nusunusu, Nai alisema hajafunga ndoa kama watu wanavyodai, bali yeye ana saluni, hivyo kujilemba ni jambo la kawaida.


“Yaani wakiona umetupia picha tu, wanaanza kuijaji. Mimi nimepaka piko kama urembo, yaani nilikuwa naonyesha kazi yangu kwa sababu mimi najihusisha na urembo, maana nina saluni, basi wao ndio wakajua mimi nimeolewa! Ni mapema mno mimi kuwa na mahusiano kwa kuwa nimetoka kuachana na Moni muda si mrefu, sasa hivi natafuta hela tu,” alisema Nai.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment