Breaking

Sunday, May 17, 2020

Rostam Kipaji, Shule , na Ubunifu

“HOI naona mtandao unakatika, huko kimya mkato au kundi limevunjika…Eeh na utanyooka raundi hii na hivyo huwezi bila mimi…Unajikuta Jay Z, oya unarudi lini?Kaka huku wamefunga mipaka ila tiketi nirudi baada ya Pasaka…

”Hii ni sehemu ya mashairi konki ya ngoma mpya ya Kaka Tuchati kutoka kwa Rostam ambayo yamejaa ubunifu wa kutosha ndani yake.

Ni ukweli usiopingika kwamba, Rostam ni bonge moja la kemistri ya Roma na Stamina ambayo inapendwa zaidi ndani na nje ya Bongo.Hawa jamaa wakiachia mkwaju huwa unakamata kinoma. Unakumbuka ngoma zao kama Kijiwe Nongwa, Hivi Ama Vile, Kibamia, Parapanda na nyingine kibao ambazo zimetikisa mno kwenye YouTube na mitandao mingine, ambako wamejizolea watazamaji wa kutosha na ilikuwa ni hatari tupu!Ghafla tu, sasa wamekamata indastri na mkwaju wao unaotisha wa Kaka Tuchati.

Katikati ya janga la Corona, mkwaju huu umesimamisha mitandao ya kijamii kutokana na majibizamo yao wakati huu ambapo Roma yupo Marekani na Stamina yupo Bongo.

Ni Kichupa ambacho kwa sasa kinapeperuka vilivyo YouTube kwa kutazamwa na watazamaji zaidi ya laki saba na nusu ndani ya siku tatu na kukamata trending namba moja, jambo ambalo limesababisha ngoma zote za wasanii wakali kupisha maana moto wake ni mkali balaa.

KIPAJIWatu wa dini huamini kuwa, kipaji mtu hupewa na Mungu katika uumbaji. Ni sehemu ya uwezo wa kufanya jambo fulani kwa ngazi ya juu. Kipaji kinaweza kuwa cha kimwili au cha kiakili.Kipaji ni uwezo wa kuzaliwa nao wa kufanya kazi fulani, lakini kinaweza kikaendelezwa au kutoendelezwa.

Kipaji hakirithishwi wala huwezi kujifunza sehemu yoyote.Ni uwezo, ujuzi ulioendelezwa, maarifa au uhodari na mtazamo alionao mtu.Asili ya ndani ya kipaji ni kuonesha ujuzi na mafanikio ambayo huwakilisha maarifa au uwezo unaopatikana kupitia kujifunza.

Kipaji huweza kuishi ndani ya mtu bila kupotea. Kadiri kinavyozidi kutumiwa ndivyo huzidi kuimarika.Rostam wamejaaliwa kuwa na vipaji ndani yao, kwani wamekuwa wakifanya muziki ambao umejengwa na maarifa ndani yake.

Uhodari katika mitazamo yao ndiyo imefanya ngoma zao kuonekana imara zaidi, kwani wamekuwa wakizungumzia uhalisia wa mashairi ambayo wanayaimba ndani yake.

Katika ngoma zao ambazo wamekuwa wakiachia, hakika ukizisikiliza unaamini hawa jamaa wana vipaji ambavyo ndani yake kuna ujuzi wa kile ambacho wanakifanya siku zote na ndiyo ikawa sababu hata kichupa chao kipya kutingisha vilivyo katika indastri ya burudani, maana ndani yake yamejaa maarifa na akili.

SHULEShule ni mahali ambapo watu hujifunza mambo mengi ambayo huwasaidia katika kuyakabili maisha hata kupata elimu juu ya jambo fulani.

Elimu hiyo ndiyo itakayomsaidia mtu kutatua jambo hilo.Watu wengi husema kwamba elimu haina mwisho, wakimaanisha kuwa elimu inaweza kutolewa kwa watu wote bila kujali kama ni watoto, vijana hata wazee. Rostam wamejaaliwa na Mungu kuwa na elimu nzuri mbali na muziki wanaofanya.

Ibrahimu Mussa ‘Roma Mkatoliki’, baada ya kumaliza elimu yake ya msingi, alikwenda kusoma Shule ya Sekondari ya Usagara kwa miaka minne kisha kuchaguliwa kwenda Shule ya Sekondari ya Old Moshi.

Aliwahi kuwa mwalimu wa Manza High School, jamaa ana Shahada ya Sayansi ya Computer aliyoipata Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM).Bonventure Kabogo almaarufu Stamina a.k.a Shorwebwenzi, amesomea Shahada ya Industrial Relations katika Chuo Kikuu cha Ustawi chenye maskani yake pale Kijitonyama-Posta jiji Dar kabla ya kutekwa na muziki wake.

Kwa hiyo unapozungumzia Rostam, unazungumzia digrii mbili!UBUNIFUWatu wengi wamekuwa wakijiuliza na kudhani kuwa ubunifu huletwa na kufanywa na watu waliokwenda shule pekee. Hii siyo kweli.Neno ubunifu linasimama katika maana ya kufanya vitu nje ya mazoea na utaratibu wa kufanana.

Ukijua namna ya kufanya kitu kilekile kwenye njia tofauti, tayari wewe tunakuita mbunifu.Rostam wamekuwa na ubunifu wa hali ya juu katika ngoma zao, ila kubwa kuliko ni ubunifu uliofanyika katika ngoma ya Kaka Tuchati.

Ubunifu wa mashairi umekuwa ni wa kitofauti, kwani wameweza kutumia misamiati yenye utamu wa maneno. Mfano; Tanga nimewavulia kofia hadi sanitizer zao zina hiliki, ukijipaka unanukia!

Video ya ngoma hiyo imefanyiwa ubunifu wa kitofauti ambao kila mtu aliyetazama ngoma hii amebaki na maswali mengi na kutaka kurudia kuitazama.Jinsi walivyokuwa wakichana kwa njia ya kuchati, hiyo imeleta ladha ya kipekee.

Mrembo aliyekuwa akikatiza mbele ya Stamina kipindi anajirekodiambaye anaonekana ni mjamzito, imewafanya watazamaji wa kichupa hicho kujiuliza mara mbili kuwa yule ni nani? Wakati inajulikana kuwa Stamina ameachana na mkewe kwa muda sasa.Hii itafanya kuongeza watazamaji wengi katika kichupa hicho kutokana.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment