Breaking

Wednesday, May 20, 2020

Sanchi Awapa Somo Wanawake "Kabla Mwezi Mtukufu Aujaisha Tusiache Kuomba Tupate Mume Bora"


Mwanadada mwenye figa matata Bongo, Janey Rimoy maarufu Sanchi ama Surraiya baada ya hivi karibuni kuslimu na kuwa Muislamu, ametoa ujumbe maalumu kwa mabinti kama yeye wakati Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaelekea kukamilika.

Sanchi aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia mitandaoni, kwenye ukurasa wake wa Instagram, amewasisitiza mabinti kutumia kipindi hiki cha mfungo kuomba ili kupata mume mwema.

“Mabinti wenzangu katika imani siku zilizobaki kabla mwezi mtukufu hujaisha tusiache kumuomba Allah aliyetukuka atupe sote mume bora. Mume mwenye kheri na mcha Mungu, mume atakaekupenda na kukuheshimu na kuiongoza familia vizuri kwa ajili ya Allah,” ameandika Sanchi

Itakumbukwa, Aprili 24 mwaka huu, #Sanchi alislimu na kuwa Muislamu ambapo hivi sasa jina lake ni Surraiya.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment