Breaking

Tuesday, May 5, 2020

Selasini Atoa Sababu Za Kuingia Bungeni Licha Ya Katazo La Chama Chake

Selasini Atoa Sababu Za Kuingia Bungeni Licha Ya Katazo La Chama Chake
Baada ya kuonekana bungeni wakati wa katazo la chama chake (CHADEMA) mbunge wa Rombo Joseph Selasini amesema alienda bungeni kwakua hakuwa na  ruhusa ya spika ya kutohudhuria vikao vya bunge kama kanuni zinavyoeleza

Selasini alikuwa sehemu ya wabunge watatu tu wa CHADEMA walioingia bungeni jana ikiwa ni siku ya kwanza baada ya katazo la chama kwa wabunge wake kuingia bungeni kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19

“Kanuni ya Bunge inaeleza wajibu wa Mbunge ni kuhudhuria vikao vya Bunge na Kamati, na Mbunge akiwa na udhuru ni lazima apate ruhusa ya Spika, Mh Naibu Spika, mimi niko hapa kwa sababu sina ruhusa na niko hapa kwa sababu naujua wajibu wangu” amesema

Wabunge wengine wa CHADEMA waliohudhulia vikao vya bunge ni Peter Lijualikali (Kilombero) na David Silinde (Mbozi)

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment