Breaking

Tuesday, May 12, 2020

Silinde " Mbowe Chama Kimemshinda....Wamefanya Maamuzi ya Kitoto Sana"

David Silinde ambaye leo hii amefukuzwa uanachama na CHADEMA amesema amesikia kufukuzwa kwake kwenye vyombo vya habari na kilichomshangaza ni uamuzi huo ambao anaweza kuuita wa kitoto

Amesema uamuzi huo uliochukuliwa na CHADEMA anaweza kusema ni wa kitoto kwasababu huwezi kumfukuza kwenye chama mtu ambaye hujamuita na kumpa mashtaka yake

Ameongeza, “Haya mambo yote nilitakiwa kuambiwa na kuelezwa kosa langu kwa maana kuna utaratibu wa kujieleza na kumuhukumu Mbunge. Huo utaratibu wote haujafanyika”

Ameeleza, “Haya ndio mambo yote tumekuwa tukiwaeleza Wananchi kuwa udikteta unaofanyika ndani ya vyama vya Upinzani watu hawawezi kujua hususan chama chetu (CHADEMA)”

Aidha, amesema kuwa kwenda Bungeni walienda kuwakilisha Wananchi na Wananchi wa Momba (Jimboni kwake) wanashangaa kuwa amefukuzwa uanachama kwasababu alienda kuwatetea Wananchi

Amemalizia, “Nafikiri Mwenyekiti Mbowe ajitafakari upya chama kimemshinda ni wakati wake a kuachia ngazi kuwaachia watu wengine waweze kukijenga”

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment