Breaking

Tuesday, May 12, 2020

Spika Ndugai Acharuka "Hakuna Mbunge Aliyefukuzwa Ubunge..Vikao vya Majungu Havifanyi Kazi"

Baada ya Kamati Kuu ya CHADEMA kukaa na kuamua kuwafukuza uanachama Wabunge wanne waliokiuka taratibu za chama hicho kwa kuhudhuria vikao vya Bunge tofauti na kilivyoamua Spika Ndugai awataka waliofukuzwa kutokuwa na hofu

Spika Ndugai amesema "Wabunge mnaapishwa na Spika na karibia wote humu nimewaapisha mimi mwenyewe sasa Wabunge niliowaapisha wala msiwe na wasiwasi hakuna cha nini wala nini vikao vya majungu hivyo havifanyi kazi"

Amesema, "Eti mmoja katika nchi hii anajifanya yeye ana mamlaka ya kufukuza Wabunge anavyotaka. Hivi nani jina lake huyo? Hii haiwezekani bwana. Haiwezekani hiyo biashara itaishia huko huko ila sio Tanzania. Tanzania hapa huwezi kujenga ufalme wa namna hiyo”

Ameongeza, “Yaani unafanya unavyotaka, Wabunge kushoto, kulia geuka sawa. Haya inama, nyanyuka. Mbunge ukipata mshahara lete sehemu fulani ya mshahara, lete huku. Wananchi mnachagua Mbunge halafu awe mtumwa wa mtu? Kweli? Akihudhuria kikao cha Bunge adhabu yake ni kufukuzwa? Hila jambo halipo”

Amesisitiza "Wale mnaoendelea kuhudhuria endeleni tutawalinda wala msiwe na mashaka kwa sababu hakuna jambo lolote mmefanya kinyume na sheria halipo kabisa. Na msajili tazama vyama vya namna hii”

Aidha amemalizia kwa kusema “Sijui kwa kuwa yeye mwenyewe anaona Novemba harudi hapa sasa anawaharibia wenzake. Mambo magumu haya ila sio magumu kihivyo

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment