Breaking

Saturday, May 9, 2020

Ummy: Takwimu za corona zitatolewa maboresho ya maabara ya taifa yakikamilika

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Serikali itaende- lea kutoa takwimu za mwenendo wa corona nchini baada ya kuka- milika kwa maboresho ya kiufundi ya katika Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii.

Alisema hayo wakati akizindua kituo cha Afya cha huduma kwa wateja (Afya call center) kilichopo eneo la Chuo cha Afya ya Sayansi ya Jamii Muhimbili (MUHAS), upanga Dar es Salaam.

“Takribani siku saba sasa hatukuweza kutoa taarifa za takwimu za maabara kuhusu mwenendo wa corona nchini
kwa sababu sasa hivi tunafanya maboresho ya maabara ya taifa ya afya ya jamii, hivyo niwatoe hofu wananchi kwamba ndani ya siku chache zoezi litakamilika na tut- aendelea kutoa taarifa kwa umma mara kwa mara”, alisema.

Ummy alisema Corona ipo
na itaendelea kuwepo kwa miezi kadhaa nchini hivyo wananchi wanapaswa kujua namna ya kuishi na ugonjwa huo kwa kujikinga.

“Ninawasihi wananchi muondoe hofu na muendelee kuchukua tahadhari ya kujikinga kwani ugonjwa wa corona bado upo Tanzania, wagonjwa wapo na vifo vinavyotakana na COVID-19 vipo, ni muhimu kutambua kuwa ugonjwa huu utaendelea kuwepo kwa miezi kadhaa hivyo lazima mchukue tahadhari ya kujikinga kama magonjwa mengine,”alisema Ummy.

Ummy aliwataka wananchi kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa za kila siku pamoja na kuchukua tahadhari kwa kue- puka mikusanyiko isiyo ya lazima, kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka, na kukaa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu mwingine.

Kuhusu vvaaji wa barakoa, aliwataka wananchi kuendelea kuvaa za vitambaa ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo na kuwa barakoa za viwandani zi- achwe zitumike kwa ajili ya watoa huduma za afya.

Amewashauri wananchi kufua na kupiga pasi barakoa za vitambaa kabla ya kuzitumia na kusisitiza kuwa zinapaswa kuw a safi kabla ya kuvaliwa.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment