Breaking

Sunday, May 17, 2020

Uwezi Amini Naibu Waziri Juliana Shonza Aipa TANO Ngoma ya ROSTAM "Kaka Tuchati, Goma Nimelielewa Sana"

Uwezi Amini Naibu Waziri Juliana Shonza Aipa TANO Ngoma ya ROSTAM "Kaka Tuchati, Goma Nimelielewa Sana"

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza amemaliza bifu na kuwapa ushauri wanamitindo Calisah na Ben Breaker pia amesema ameilewa ngoma mpya ya kundi la Rostam "kaka tuchati".Akizungumza kwa njia ya simu kupitia show ya "Friday Night Live" ya East Africa TV, Naibu Waziri alianza kuwapa ushauri wanamitindo hao ambao walikuwa wana bifu siku za nyuma, kisha akamalizia kwa kusema ameilewa ngoma ya kaka tuchati.

"Niwapongeze kwa kuwakutanisha hao vijana wetu wawili, nafikiri sisi kama Wizara ambayo tunasimamia kazi za sanaa naona tasnia ya ubunifu na uwanamitindo bado ni changa hapa kwetu na inakua, kwa hiyo waliokuwepo wanahitaji kuunganisha nguvu ya pamoja ndiyo maana nikawasisitiza huu sio wakati wa malumbano na kuangalia nani mkubwa nani mdogo" ameeleza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo

Aidha katikati ya mahojiano hayo akamalizia kwa kusema msalimie Stamina namuona hapo, goma nimelielewa sana kaka tuchat.

Mahojiano kamili tazama kwenye video hapa chini.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment