Breaking

Saturday, May 16, 2020

Vita Kati Ya H.Baba na Diamond Platnumz Yafika Patamu


Vita kati ya msanii wa muziki wa BongoFleva Hamis Baba 'H.Baba' dhidi ya Diamond Platnumz imezidi kushika kasi baada ya msanii huyo kuchapisha post katika mtandao wa kijamii na kutafsiriwa kama dongo kwa Diamond Platnumz.

H.Baba ambaye alitamba na nyimbo mbalimbali mwanzoni mpaka mwisho mwa miaka ya 2000 aliandika: "Sicheki nawapiga show za bure tena mnaomba mkaimbe bure mwisho wa siku mnaimba remix nyimbo za watu au zako hawazijui eti mnaitangaza Tanzania unaimba wimbo wa Mkongo unasema wa kwako huo ndio wimbo bora wa mwaka huu show yako umearikwa wewe imba nyimbo zako remix za nini?

Hivi karibuni H.Baba amekuwa akiwasakama wasanii na wafuasi wa WCB Wasafi hususan Diamond Platnumz kutokana na ukarabu wake na Harmonize, ambaye kwa sasa hana uhusiano mzuri wa lebo hiyo

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment