Breaking

Friday, May 22, 2020

Wanafunzi Form Six Watakiwa Kuripoti May 30


Leo May 22, 2020 Wizara ya Elimu imewataka wanafunzi wa kidato cha sita wale wa shule za bweni kuanza kuripoti Mei 30 mwaka huu.

Waziri mwenye dhamana ya Elimu nchini Profesa Joyce Ndalichako amesema hayo leo jijini Dodoma.

“Wanafunzi wa kidato cha sita watafungua tarehe 01/06/2020 na wanafunzi watakuwepo shuleni wakijisomea na kufanya maandalizi ya mitihani mpaka tarehe 28/06/2020” Prof. Joyce Ndalichako.

“Mitihani ya kidato cha sita itaanza rasmi tarehe 29 Juni na itafanyika hadi tarehe 16 Julai 2020, mitihani hiyo ya kidato cha sita itaenda sambamba na mitihani ya ualimu”. Prof. Joyce Ndalichako

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment