Breaking

Sunday, May 17, 2020

Waziri Nchemba Amcharua Zitto KABWE Kutaka Majibu ya Uchunguzi wa Maabara "Uko Bize Kupandikiza Chuki"

Waziri wa Katiba na Sheria, Mwigulu Nchemba, amemcharua kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe huku akimuambia kamati iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza maabara ya kitaifa hakuiunda yeye.

Jana Zitto alisema kuwa Rais John magufuli alitangaza maabara ya taifa haitoi vipimo vya kweli vya Covid-19

Kiongozi huyo aliitaka serikali kutoa majibu ya uchunguzi uliofanywa katika maabara hiyo na sio kukaa kimya.

Nchemba alimjibu zitto kuwa “Zitto, kamati hukuunda wewe! Tor hukutoa wewe! Busy kutaka report, mko busy kuwadodosa wajumbe wa tume, kupanda chuki,” aliandika Nchemba.

Nchemba amesema Watanzania kila siku wanapata huduma mahospitalini ” wewe unataka mpaka tupime mashine ya mapapai?,”.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment