Breaking

Tuesday, May 19, 2020

‘We Are Just Friends.’ Ali Kiba Akataa Madai ya Kuwa Uhusiano wa Kimapenzi na Hamisa Mobetto

Uvumi umekuwa ukienea sana katika mitandao ya kijamii kuwa msanii wa bongo Ali Kiba na video vixen Hamisa Mobetto wamo katika uhusiano wa kimapenzi.

 Madai hayo yaliibuka siku chache baada ya Ali Kiba kutoa wimbo wake wa ‘dodo’. Msanii huyo alikataa madai hayo na kusema kuwa ni marafiki tu hamna cha kuongeza wala kupunguza.

Alitoka kwa lebo ya Alikiba, akaingia kwa lebo ya Harmonize. Ibraah atisha na ngoma mpya TZ
Alifichua kuwa walikuwa wanazungumza na Hamisa baada ya wimbo huo kutoka na kuongea mambo na biashara zingine na hata kumpongeza kwa kuwa mtu mzuri na wa maana.

“We do chat with Hamisa, it could about the song we did together. She is a nice person who makes everyone feel comfortable and made me feel comfortable too but its nothing like a love relationship and we have been friends. I would not want people to criticise us wrongly.” Alisema Alikiba.

Wawili hao walionekana wakiwa wanaucheza wimbo huo kama wapenzi. Baada ya hao kuonekana hadharani uvumi ulianza huku wengi wakitaka majibu kama wawili hao ni wapenzi.

Wimbo huo alioutoa, Ali alikuwa amevalia kama mfalme na Hamisa kama malkia.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment