Breaking

Friday, May 15, 2020

Wengi Wanamkubali Bob Marley ila Mfalme wa Reggae Duniani ni Lucky Dube

Dunia yote inamtukuza na kumuhusudu Bob Marley (Culture?) kama mfalme wa muziki rege, sijui wanatumia vigezo gani hasa. Wanamshusha na kumchukulia poa Lucky Dube sijui kwakua Bob aliuawa ndio wanakua na sympathy naye.

Kwa upande wangu japo Dube alimuheshimu Bob ila kwangu dube ndio mfalme wa muziki wa rege duniani. Nyimbo safi zenye ujumbe mwanana, beats zilizoenda shule performance za hadhi ya nyota 15 alizofanya! Nina uhakika Bob angekuwepo wakati Dube Anatoa Album zake 3 za mwanazo (hasa Slave) angempigia magoti Dube na kumsujudu kwa nyimbo bora alizotoa.

Huyu jamaa anajua hasa sikiliza nyimbo zake zote 80% lazima uzipende tu, ukutaka ujue ukali wa huyu mtu angalia Live performance zake utadata.

Najua mtanipinga humu na kunipopoa ila kwangu huyu ndio nishampitisha kua Mfalme wa Rege Duniani, hakuna mwingine.

Ninauhakika huko alipo kapumzika kwa amani maana katimiza kile kilichomleta duniani (Kuhamasisha watu waamke) japo alikua na mapungufu yake kama mtu yoyote yule ila naamini huyu mtu mbingu ni yake na tunaweza mwita mtakatifu kwa kazi yake nzuri.

Sikiliza hizi;

 HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment