Breaking

Monday, June 15, 2020

Bilnass Anawivu Balaa...Unaambiwa Nandy Apigwa Biti Kali Asiwe Karibu na Willy Paul


Unaukumbuka ukaribu wa mahusiano ya kazi kati ya msanii Nandy na Willy Paul kutoka nchini Kenya ambavyo ulivyoleta utata kwa watu kuhusu kuwa kwenye mahusiano.


Sasa stori zinaendelea ni kwamba Nandy amepigwa biti na mpenzi wake Billnass kuhusu kuwasiliana na Willy Paul, ambao wameshafanya kazi mbili ambazo ni njiwa na halleluya.

Akizungumza suala hilo la kupigwa biti la kuwasiliana naye kwenye Friday Night Live ya East Africa TV inayoruka kila siku ya Ijumaa kuanzia 3:00 hadi 5:00 usiku, Nandy amesema

"Marafiki zangu wote wa kiume naongea nao,  hata Billnass pia huwa anaongea nao, kwangu hakuna mwanaume yeyote ambaye nimefanya naye kazi halafu nisiambiwe kama tuna ukaribu au tupo kwenye mahusiano, hata kwa Aslay na Ommy Dimpoz ilikuwa hivyohivyo, mwenye mahusiano ambaye nimewahi kufanya naye kazi ni Billnass tu, na tulianza mahusiano kabla sijawa Nandy huyu wa sasa"


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment