Breaking

Friday, June 5, 2020

Clouds FM ilivyomuandaa Kennedy kwa Ajili ya Kuchukua Nafasi ya B Dozen

By Sangu Joseph

Kama.nilivyoahidi kwenye kwenye Andiko langu lililopita kuwa ningeandika kuhusiana na kuathirika au kutoathirika kwa Clouds FM kuondoka Kwa BDozen nadhani ule wakati ndiyo leo.
.
Ukiniuliza binafsi je Sangu J unadhani Clouds watayumba baada ya kuondoka kwa BDozen nitakwambia BIG HAPANA ila watapata ushindani mkubwa kwa sababu hawa jamaa huwa wanakua na tahadhari ya kuwandaa Watangazaji wao wapya, wachukue nafasi pindi Watangazaji wa muda mrefu wasipokuwepo, ndiyo maana kwenye siku ambazo ni sherehe za Kitaifa mara nyingi unasikia sauti mpya, kama wakina John Jackson, Lugha Kali, Abdul Chambea na MoJ360, Broh Tei The Best, Perfect Crispin.
.
Turudi kwa Dozen na Clouds kwanini nasema hakuna Pengo, hawa jamaa walianza kumuandaa Kennedy The Lemedy, kumrithi Dozen muda mrefu ndiyo maana uliona alipewa mashavu mengi sana kwa muda mfupi Wadau tunasema waliamua kumpeleka Mjini.

Nawakumbusha kwanza Kennedy alipewa kitu kinaitwa Waziri wa Burudani kwenye Fiesta, lengo lilikua ni kumjengea heshima kama aliyokuwa nayo Dozen kwa wasanii, ili upate Shavu la kuperfom Fiesta ilikua lazima upitie Kwa Kennedy, hakuishia hapo Mara Paap akaoneka kama Mwakilishi wa Vijana kwenye Fainali ya Miss Tanzania ili kumtambulisha kwa Wadada na kumjengea kizazi chake cha Warembo, baada ya hapo akaonekana kwenye kampeni ya Kipepeo kama Balozi yeye na Meena Ally, lengo ni kumtambulisha Kennedy kwenye kizazi kipya kinachosikiliza Radio mtaani ambao wengi wao ni Vijana wa baadaye na wao ndiyo hitaji lao, unajua Taaluma ya Utangazaji huwa zina nyakati, kuna nyakati unakua juu Ila hicho kizazi kikipita utashuka, sasa utakua media kama Clouds wanalijua hilo Kwamba Dozen alianza 2000 kutangaza maana yake Vijana wa 2000 - 2010 wengi sasa ni watu wazima na kusikiliza Radio ni mara chache sana hivyo Kennedy inabidi apelekwe Mjini awachukue Vijana kuanIa 2016 - na kuendelea kwa sababu ni mwenzao na wanamuelewa.
.
Ukiangalia wakati wa kipindi Kennedy alikuwa ni mtu anayekaa karibu zaidi na Dozen kuliko Watangazaji wote XXL, na hata sasa unaona yeye ndiyo kama Main Man kwenye Show, anacontrol kila kitu.
.
So kuondoka kwa Twangalla na uwekezaji wa Clouds kwa Kennedy ni suala la muda na kusubiri, nikiri Heshima ya BDozen kwenye Burudani itabaki kuwa juu juu zaidi.

Wakati ujao nitaeleza maoni yangu juu ya namna ambavyo nadhani Boss @Majizzo atamtumia BDozen #DozenAmetua pale uswahilini Efm na TV - E
.
Nicheki Instagram : Twit : FB Sangu Joseph
.
#KijanaMzalendo #IloveT

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment