Breaking

Monday, June 15, 2020

Kangi Lugola 'Rais Magufuli Amekuwa Kama Yesu Kristo Watanzania Wanamlilia na Kumfuata"


Mbunge wa Mwibara kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Kangi Lugola, amesema kuwa watu kama Rais Magufuli hauwezi ukawapata popote pale na ndiyo maana hata alipoamua kumtengua kwenye nafasi yake ya Uwaziri alimshukuru na hivyo kumfananisha na Yesu Kristo.


Lugola ameyabainisha hayo leo Juni 13, 2020, Bungeni Dodoma wakati akichangia hoja ya Bajeti katika Mkutano wa 19, Kikao cha 45.

"Rais Magufuli amekuwa kama Yesu Kristo, Watanzania wanamlilia na kumfuata na ndiyo maana hata aliponitengua nilisema, ulinipa heshima ya huu Uwaziri na leo umetwaa Uwaziri ulio wako, jina la Magufuli libarikiwe, tunapokuwa na Rais kama huyu hatutakiwi kuingia kwenye mijadala ya kumtafuta mwingine" amesema Kangi Lugola.

Aidha Kangi ameongeza kuwa "Niliwahi kusema watu wa namna kama ya Rais Magufuli hawazaliwi kila wakati na hauwezi kuwapata kila mahala, watu ambao unaweza kuwapata kila mahala ni walevi kama kina Mbowe na habari ya mjini sasa hivi ni alilewa na kuvunjika mguu, na Rais Magufuli ninamfananisha kama Mwenge wa Uhuru".


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment