Breaking

Wednesday, June 17, 2020

Nikki Wa Pili Aichambua Miaka Mitano ya Magufuli

Nikki Wa Pili ni msanii wa HipHop kutoka Weusi, pia jina lake linatajwa sana kuwa miongoni mwa wasanii wanaojihusisha na masuala ya kisiasa, kutokana na ushawishi wake kwenye jamii, vijana na maendeleo kwa ujumla.


Sasa kupitia EATV & EA Radio Digital, msanii huyo ametaja vitu alivyoviona kwenye uongozi wa miaka mitano wa Rais Magufuli, ambapo hii leo amelivunja rasmi Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Kuna vitu ambavyo amevifanya na havikuwepo kabla ya hapo, kwa mara ya kwanza kumekuwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, tulikuwa hatunaga hiyo wizara, pili kumetokea msukumo wakutengeneza umoja wa Taasisi kutoka COSOTA na BASATA, mwanzo COSOTA ilikuwa ipo Wizara ya Biashara na BASATA ilikuwa Wizara ya Habari, tatu kumekuwa na mchakato wa kutengeneza sera mpya ya sanaa na burudani ambayo itatizama kama biashara" ameeleza

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment